Connect with us

Soka

Ronaldinho Aachiwa Gerezani

Staa wa soka duniani Ronaldinho Gaucho hatimaye amefanikiwa kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa kwa siku 32 kwa kosa la kukutwa na pasipoti ya kusafiria ambayo ni feki.

Staa huyo alikamatwa mwezi uliopita akiwa na kaka yake Roberto Asis na kupelekwa gerezani ambapo alikua akitumia muda mwingi kucheza mpira na wafungwa nchini humo.

Gustavo Amarilla ambaye ni jaji nchini humo ameamua watu hao kutoka gerezani japo wataendelea kuwa chini ya ulinzi maalumu katika hoteli watakayokaa mpaka hapo mashtaka yake yatakapoamuliwa rasmi baada ya upelelezi kukamilika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka