Connect with us

Soka

PSG Yashinda,Neymar Akila Umeme

Licha ya kutanguliwa kufungwa bao moja timu ya Paris St.German ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Bourdeaux katika mchezo wa ligi kuu nchini Ufaransa(Ligue 1).

mchezo ulimalizika kwa jumla ya magoli saba kufungwa na kuacha swali kwa kocha wa PSG kuhusu uwezo wa timu yake kuzuia.

Edson Cavan aliifungia PSG bao la 200 akisawazisha bao la Hwang Ui-jo huku Marquinhos aliyeingia kuchukua nafasi ya Thiago Silva aliyeumia dakika ya 25 akifunga mabao mawili na Kylian Mbappe akimalizia goli la nne.

Neymar alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Yacine Adli na mwamuzi kumuonyesha staa huyo kadi nyekundu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka