Connect with us

Soka

Psg 3,Di Maria Apiga 2

Timu ya Paris St Germans imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya (Uefa) uliofanyika wa Parc de paris jijini Paris nchini Ufaransa.

Shujaa katika mchezo huo alikua na Muargentina Angel di Maria aliyefunga mabao mawili dakika ya 14 na 33 huku akifanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa katika kusukuma mashambulizi katika idara ya kiungo akisaidiana na Idrisa Gueye.

Katika mchezo huo Psg iliwakosa Neymar Edson Cavan na Kylian Mbappe kutokana na majeraha lakini hiyo haikusababisha kutompa presha kocha Zinedine Zidane ambaye alishuhudia mabao mawili ya timu yake yakikataliwa na mwamuzi Anthony Taylor huku Thomas Meunier akifunga bao la tatu dakika ya 90+4.

Kipigo hicho kinazidi kumuweka matatani kocha Zinedine Zidane ambaye alifanikiwa kuipa mataji matatu ya ulaya mfululizo timu hiyo baada ya kuichukua kutoka kwa mreno Jose Mourinho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka