Connect with us

Soka

Presha Yaikimbiza Yanga Dsm

Kufuatia presha ya mashabiki timu inapocheza jijini Dar es salaam klabu ya Yanga imeamua kuhamishia michezo yao ya kimataifa jijini Mwanza ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Pyramids ya nchini Misri.

Akiongea na waandishi wa habari,makamu mwenyekiti wa klabu hiyo David Mwakalebela amesema licha ya sababu hiyo pia uwepo wa michezo ya ligi kuu mkoani humo baada ya mechi hiyo ya kimataifa ni sababu nyingine iliyowasukuma kuhamishia mechi hiyo jijini humo pia kutoa hamasa kwa mashabiki wa kanda ya ziwa.

Yanga itavaana na Pyramids katika kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika mchezo utakaochezwa oktoba 27.

“Moja, ni kukwepa presha ya mashabiki ambayo imekuwa ikijitokeza kila wanapocheza mechi zao za ligi ya michuano hiyo ya kimataifa, hivyo kama uongozi tunaamini vijana wetu watacheza bila ya presha Uwanja wa CCM Kirumba.

Kabla ya kucheza na Pyramids timu hiyo itacheza na Alliance fc katika uwanja huo huo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara hivyo kutoa nafasi ya kuzoea uwanja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka