Connect with us

Soka

Pondamali Afunguka Kuondoka Yanga

Pengine ni kinyume na watu walivyokua wanafikiri kuwa kocha Juma Pondamali alitimuliwa katika klabu ya Yanga sc lakini kocha huyo ameamua kufunguka ukweli juu ya kuondoka kwake.

Kocha huyo mwenye mbwembwe na mpenzi wa mziki wa dansi alisema kuwa hakufukuzwa klabuni hapo bali yeye mwenyewe aliomba kuondoka baada ya kuongea na mwenyekiti wa klabu hiyo Dk.Mshindo Msolla ambapo alimfungika mipango ya timu hiyo kwa msimu huu nan ndipo aliomba kuondoka ili apate stahiki zake.

“Baada ya kukubaliana na Msolla niliamua niondoke ili nipate stahiki zangu kwa maana nilifahamu timu haiwezi kufikia malengo yake na benchi la ufundi lingetimuliwa kabla ya msimu kuisha jambo ambalo lilitokea baadae”.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka