Connect with us

Soka

Nonga,Lipuli Watibuana

Nahodha wa klabu ya Lipuli Fc Paul Nonga hajajiunga na kambi ya timu hiyo kufuatia kutomaliziwa malipo yake hasa mshahara na dau la usajili la mkataba wa sasa.

Straika huyo aliyecheza timu kadhaa nchini Ikiwemo Yanga sc,Mbeya city na Mwadui Fc alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Lipuli Fc ambao unaisha mwishoni mwa msimu huu.

“Ni kweli sijaripoti kambini lakini sijagoma ila kuna mambo ya kimkataba ambayo hayaja timizwa. Sijalipwa mshahara wa miezi mitatu pia dau langu la usajili sijamaliziwa na niliuambia uongozi wanalipe hata nusu lakini mpaka sasa naona ni kimya,”  Alisema Paul Nonga, Nahodha wa Lipuli FC.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka