Connect with us

Soka

No Kiporo-Wambura

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura ametoa onyo kwa vilabu hususani klabu ya Yanga kutoomba kusogeza mbele michezo ya ligi ili kuepuka mkanganyiko wa ratiba pasipo na sababu za msingi.

Wambura amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisisitiza kuwa klabu hiyo ambayo imeomba kusogezwa kwa mechi yake dhidi ya Polisi Tanzania kwa kuwa imechelewa kuwasili nchini ikitokea Zambia ilipokwenda kucheza na Zesco United ambapo ilitolewa kwa jumla ya magoli 3-2.

“Sambamba na hilo, tunatoa onyo kwa Klabu ya Yanga na klabu nyingine yoyote kuacha hii tabia ya kuomba michezo yao isogezwe mbele bila sababu za msingi kwani hii tabia ikiendelea itatuletea mkanganyiko huko mbele,” alisema Wambura.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka