Connect with us

Soka

Niyonzima Kuivaa Kagera Sugar

Daktari wa klabu ya Yanga, Docta Shecky Mngazija amesema kiungo wa Klabu hiyo Haruna Niyonzina hajaumia Sana hata leo anaweza kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar mchezo ambao utafanyika alhamisi ya July 09.

Niyonzima aliumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United uliofanyika mjini Musoma ambapo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulaziz Makame,Mchezo ambao ulimalizika kwa sare.

Kuumia kwa kiungo huyo maestro kumeleta taharuki kuelekea mchezo wa watani wa jadi utakaofanyika Julai 12 jijini Dar es salaam katika mchezo wa nusu fainali kombe la shirikisho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka