Connect with us

Soka

“Nimeimarika Zaidi”-Lukaku

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, amesema kuwa kwasasa ameimarika zaidi tangu alipo hamia Inter Milan kutoka Manchester United.

Akizungumza na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry kupitia Instagram Live, Lukaku alisema, anafanya kazi yake kwabidii kuhakikisha kuwa anakuwa bora zaidi.

Lukaku ambaye aliuzwa na united kwa takribani pauni Milioni 73 alimwambia Henry”Unapoimarika sio tu juu yako mwenyewe, kufunga magoli ndio dawa yangu, kitu ambacho kipo ndani ya moyo wangu. Lakini bado naendelea kujifunza. Nadhani nataka kuisaidia timu yangu, natakiwa kuwa nauwezo wa kutoa msaada huo.”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka