Connect with us

Soka

Nigeria Wapoza Machungu Afcon

Hatimaye timu ya taifa ya Nigeria(Super Eagles) imepoza machungu ya kufungwa nusu fainali baada kuibuka mshindi wa nafasi ya tatu katika michuano hiyo ambayo fainali itafanyika ijumaa ya leo kati ya Senegali na Algeria.

Nigeria ambao ni mabingwa mara tatu wa michuano hiyo walifungwa 2-1 na Algeria katika mcheza wa nusu fainali na kupata na nafasi ya kupambana na Tunisia aliyefungwa na senegali katika hatua hiyo.

Katika mchezo huo wa kutafuta mshindi wa tatu bao la nigeria lilifungwa na mshambuliaji Odian Ighalo dakika ya pili ya mchezo na kuwahakikishia Super Eagles nafasi ya tatu katika michuano hiyo.

Hata hivyo nusura Tunisia wafungwe goli la pili katika mchezo huo uliokua wa taratibu baada kufanya makosa ya kizembe na kumlazimisha golikipa Cherifia kufanya kazi ya ziada kuokoa kiki ya chukwueze  na adhabu iliyopigwaa na Samuel Kalu.

Nigeria waliokuwa wanapewa nafasi ya kutwaa kombe hilo pia wanaweza kujipoza endapo mshambuliaji wao Odian Ighalo atatwaa tuzo ya mfungaji bora baada ya kufunga mabao matano akiwaombea Sadio Manne wa senegali na Adam Ounas wa Algeria wenye mabao matatu kila mmoja wasifunge katika mechi ya fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka