Connect with us

Soka

Ni Mwendo wa 4G

Klabu ya Simba imeendeleza wimbi la ushindi baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 4 bila dhidi ya Mbeya city Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kalamu ya mabao ilifunguliwa mapema dakika ya nane na Meddie Kagere kwa njia ya penati baada ya Miraji Athuman kufanyiwa madhambi baadae dakika ya 43 Cletous Chama alifunga bao la pili akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu.

Simba ilibidi wasubiri mpka dakika ya ishirini kipindi cha pili kupata bao la tatu baada ya Shiboub kuweka mpira nyavuni akimalizia kazi ya Ajibu na dakika kumi mbele Deo kanda aliyeingia kuchukua nafasi ya Ajibu aliandika bao la nne akimalizia pasi ya Chama.

Simba imejikita kileleni baada ya kukusanya pointi 21 katika michezo nane ambapo ilipoteza mchezo uliopita dhidi ya Mwadui fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka