Connect with us

Soka

Ngorongoro Mabingwa Chalenji

Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) imetwaa ubingwa wa michuano ya kombe la chalenji kwa vijana iliyofanyika nchini Uganda baada ya kuifunga Kenya kwa bao 1-0 katika fainali iliyomalizika jioni hii.

Ngorongoro ilipata goli hilo dakika ya 46 baada ya Otieno Onyango kujifunga na mpaka mechi inamalizika Heroes ilifanikiwa kulilinda bao hilo hivyo kuwafanya kutangazwa mabingwa wa michuano hiyo huku wakiweka rekodi ya kushinda mechi zote katika michuano hiyo.

Kelvin John alifanikiwa kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga mabao 7 na kuwazidi washambuliaji wote huku akipata pia tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka