Connect with us

Soka

Ndayiragije Achomoka Azam

Kocha Ettiene Ndayiragije amejiuzulu nafasi yake ya ukocha mkuu wa klabu ya Azam fc huku ripoti zikibainisha anakwenda kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) kama kocha mkuu baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa muda.

Ettiene raia wa Burundi alikaimu nafasi hiyo baada ya aliyekua kocha mkuu Emmanuel Amunike kutimuliwa kutokana na kufanya vibaya katika michuano ya mataifa ya Afrika (Chan) yaliyofanyika nchini Misri.

Tayari klabu ya Azam imemleta aliyewahi kuwa kocha wa klabu hiyo Aristica Cioaba kuja kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na inatarajiwa mchana wa leo kufanyika hafla rasmi ya kumuaga kocha huyo na kumtambulisha rasmi Cioaba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka