Connect with us

Soka

Namungo Yatoa Dozi Nene

Klabu ya Namungo Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 6-2 dhidi ya Primera de Augosto katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa chamazi jijini Dar es salaam. 
Magoli ya Namungo yamefungwa na Hashim Manyanya (32’), Sixtus Sabilo (38’, 59’), Reliants Lusajo (55’), Erick Kwizera 66’ na Stephen Sey dakika ya 72.
Mechi ya marudiano itapigwa ndani ya saa 72 zijazo, na Namungo itahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 4-0 ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hii ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Awali mchezo huo ilibidi uchezwe nchini Angola lakini changamoto ya ugonjwa wa Corona ilisababishwa mchezo huo kuahirishwa na kuamuliwa kufanyika nchini kwa michezo yote miwili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka