Connect with us

Soka

Nafasi ya Amunike Yageuka Lulu Stars

Kufuatia kufukuzwa kwa kocha wa Taifa stars Emmanuel Amunike makocha wengi wamewasilisha wasifu wao katika shirikisho la soka la Tanzania(Tff) ili kupata nafasi ya kuinoa timu hiyo.

Kocha huyo aliyewahi kuichezea Barcelona ya hispania aliondolewa baada ya timu ya taifa kufanya vibaya katika fainali hizo zilizofanyika nchini Misri huku Stars ikishiriki kwa mara ya pili baada ya miaka 39 kupita na kutolewa kwa aibu kwa kuwa timu iliyofungwa magoli mengi zaidi.

Akiongea na vyombo vya habari katibu mkuu wa shirikisho hilo Wilfred Kidao alisema mpaka sasa makocha takribani 100 wamewasilisha wasifu katika shirikisho hilo.

“Tumepokea maombi ya makocha zaidi ya 100 wakitaka kazi ya kuifundisha timu ya taifa, maombi ni mengi na tunayafanyia kazi kwa uangalifu mkubwa, suala la kocha anayekuja kwa ajili ya timu ya taifa tunaomba watu
watulie tutapokuwa tayari tutatoa taarifa”.Alisema katibu huyo.

Stars kwa sasa ipo chini ya kocha wa muda Ettiene Ndayiragije ambaye amepewa majukumu hayo katika kuelekea kwenye mechi dhidi ya kenya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan) huku akisaidiwa na mzawa Selemani Matola.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka