Connect with us

Soka

Mwamuzi Aiua Stars

Penati ya utata dakika ya 68 imechangia kufungwa kwa timu ya taifa ya Tanzania kwa mabao 2-1 na Libya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2021.

Stars ilitangulia kupata bao dakika ya 18 likifungwa na Mbwana Samatta kufuatia Simon Msuva kuangushwa ndani ya eneo la hatari na kuipa uongozi stars mpaka kipindi cha kwanza.

Licha ya kufungwa Libya walimiliki mchezo na kufanya mashambulizi kadhaa na dakika ya 68 mwamuzi aliwapa penati iliwapa bao la kusawazisha wenyeji na baadae dakika ya 81 Anis Saltou aliipatia Libya bao la pili na la ushindi.

Kwa matokeo hayo Stars imeangukia nafasi ya tatu huku Tunisia akiongoza kundi kwa pointi 6 na stars ikitanguliwa na Libya kwa tofauti ya mabao ya kushindwa na kufunga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka