Connect with us

Soka

Msuva Aikoa Stars

Winga wa Diffaa El-Jadid ya Morroco Saimon Msuva ameisaidia Tanzania kupata sare  ya bao 1-1 dhidi ya Burundi baada ya kusawazisha goli la Cedrick Amis lililofungwa dakika ya 81.

Msuva aliipatia Stars bao hilo dakika ya 86 baada ya mabeki wa timu hiyo kujichanganya kufuatia shambulizi la kushtukiza lililofanywa na Taifa stars.

Licha ya sare hio stars ilijitahidi kukwepa hujuma baada ya kuhisi kupuliziwa dawa vyumbani hali iliyowasababisha wachezaji kwenda mapumziko kwenye mabenchi ya uwanjani badala ya vyumbani.

Mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia nchini qatar mwaka 2022 itarudiwa siku ya jumamosi septemba 8 nchini katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka