Connect with us

Soka

Mshahara Wa Banda Kufuru Sauzi

Soka linalipa ndio kauli ambayo unaweza kuisema kufuatia mchezaji wa kitanzania Abdi Banda kusaini mkataba mnono huko bondeni baada ya kujiunga na timu ya Highland Park inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika kusini.

Timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1959 inatumia uwanja wa Balfour Park Stadium unaoingiza watazamaji 13500 imemsaini beki huyo akitokea Baroka Fc ya nchini humo aliyojiunga nayo akitokea Simba sc iliyomsajili kutokea Coastal union ambayo ilimlea tangu akiitumikia timu ya vijana ya klabu hiyo.

Banda amesaini mkataba huo ambapo atakua analipwa randi 150000 ambayo ni takribani ni kiasi cha shilingiza kitanzania milioni 24 kwa mwezi kiasi ambacho ni kingi ikilinganishwa na mishahara wanayolipwa mastaa nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka