Connect with us

Soka

Mshahara Kikwazo Makambo Yanga

Imeripotiwa kwamba kiasi cha mshahara anaolipwa straika Heritier Makambo na klabu ya Horoya ndio kikwazo kikuu cha kumrudisha katika klabu ya Yanga sc.

Makambo aliuzwa na Yanga kwenda Horoya ya nchini Guinnea kwa mkataba wa miaka mitatu inaelezwa yuko tayari kurudi mitaa ya Jangwani endapo timu hiyo itamhakikishia mshahara mnono kama anaolipwa na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa kocha Mwinyi Zahera ambaye alimleta Makambo nchini amesema ni ngumu staa huyo kurejea kutokana na maslahi anayolipwa huko ambapo kwa Yanga ni ngumu kuyapata.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka