Connect with us

Soka

Mrithi wa Ndayiragije Atambulishwa Azam Fc

Klabu ya Azam fc leo imemtambulisha rasmi kocha Aristica Cioaba kama kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Ettiene Ndayiragije ambaye anakwenda kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars).

Cioaba aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo miaka miwili iliyopita ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari huku akiahidi kufanya makubwa zaidi.

“Naushukuru uongozi wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani na mimi, kikubwa mimi sio mgeni hapa naijua timu, wachezaji wananijua na pia wanafahamu falsafa yangu, jambo kubwa ni kuendelea kuifanya timu kuwa juu pamoja na kushinda mataji,” alisema.

Aidha, kama ilivyokuwa awali Cioaba, mwenye leseni ya juu ya ukocha ya UEFA Pro Licence, amerejea sambamba na Kocha wa viungo, Costel Birsan, aliyekuwa naye awali kipindi anaifundisha Azam FC.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka