Connect with us

Soka

Mourinho Kocha Mpya Totts

Klabu ya Tottenham imemteua Jose Mourinho kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Mauricio Pochetino ambaye amefukuzwa kutokana na matokeo mabaya kwa siku za hivi karibuni.

Mourinho (56) amesaini mkataba wa miaka mitatu ambao utadumu mpaka mwaka 2023 ili kuleta mataji klabuni hapo baada ya Pochetino kushindwa kuleta taji lolote tangu ateuliwe mwaka 2014 na kufanya timu hiyo kutochukua kombe lolote tangu mwaka 2008.

Pochettino amefukuzwa klabuni hapo baada ya kudumu kwa miaka mitano huku mtendaji mkuu wa klabu hiyo Daniel Levy alisema “kwa Mourinho tumepata meneja mwenye mafanikio duniani”.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka