Connect with us

Soka

Mourinho Anukia Newcastle Utd

Kocha wa zamani wa Manchester united Jose Mourinho ameripotiwa kuwaambia rafiki zake kuwa yuko tayari kujiunga na Newcastle ikiwa wamiliki wapya wa timu watamhitaji kwenda kuwafundisha wababe hao wa St.James Park.

Mourinho 56 yuko huru baada ya kufukuzwa na Manchester united Desemba mwaka jana ambapo mpaka sasa amekua akifanya kazi za uchambuzi wa mpira katika Televisheni mbalimbali Duniani.

Imefahamika Tajiri wa kiarabu Sheikh Khalid Bin Zayed Al Nehayan  yupo kwenye hatua za mwisho kuichukua klabu hiyo kutoka kwa Tajiri Mike Ashley na anafikiria kutoendelea na Kocha Rafa Benitez ili Jose Mourinho akaongeza makali katika benchi la ufundi huku ikisadikiwa watatenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya usajili.

Rafa na Mourinho wamekuwa wakipishana mlangoni toka mwaka 2010 baada ya kumrithi Mourinho Intermilan akiwa ametoka kuwapa mataji matatu likiwemo la klabu bingwa ulaya na baadaye Mourinho alienda kumrithi Rafa katika klabu ya Chelsea mwaka 2013 akitokea Real Madrid

Mourinho hajawahi kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani wa Newcastle united katika maisha yake ya soka nchini Uingereza akicheza mechi saba huku akitoka sare mara tatu huku akifungwa mara nne.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka