Connect with us

Soka

Morrison Mambo Safi Yanga

Mazoezi ya Yanga Sc yameendelea leo katika Uwanja wa shule ya sheria ambapo Bernard Morison ni moja ya wachezaji ambao wamejiunga na timu leo hii baada ya kukosekana kwa siku kadhaa kutokana na majeraha.
Mara baada ya kufika Morison aliwaomba radhi wachezaji wenzake kwa kushindwa kusafiri na timu kisha akaendelea na mazoezi ambapo alionekana kuwa fiti licha ya kutoka majeraha.
Yanga inatarajiwa kuwafuata Azam fc mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ambao utaamua hatma ya nafasi ya pili baada ya uhakika wa Simba sc kuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa. 

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka