Connect with us

Soka

Morrison Gumzo Kila Kona

Staa mpya wa klabu ya Yanga Benard Morrison ameendelea kuwa gumzo nchini kufuatia kiwango cha hatari anachozidi kuonyesha staa huyo raia wa ghana kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi.

Staa huyo aliyechezea klabu za As Vita,Dc Motema Pembe na Orlando Pirates alianza kuonyesha cheche kwenye mechi dhidi ya Singida united ambapo alifanikiwa kutoa asisti mbili na kisha kufunga na kutoa pasi ya goli la pili kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Prisons.

Licha ya kutoa mchango mkubwa katika timu hiyo staa huyo amerejesha furaha jangwana baada ya kuw kivutio kutokana na kutoa shoo ya kuchezea mpira huku akitoa pasi na kuganda kwa mbwembwe na kuwaacha mashabiki wa klabu hiyo wakitamba.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka