Connect with us

Soka

Morrison Atupwa Kakaangoni

Mchezaji wa Yanga SC Bernard Morrison amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons FC Jeremia Juma wakati mpira ukiwa umesimama kwenye mchezo uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na shirikisho la soka nchini(Tff) imesema mchezaji huyo amepelekwa kwenye kamati hiyo ambayo itakaa na kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria.

Suala la mchezaji huyo limekua na kelele nyingi hasa ikizingatiwa mechi baina ya watani wa jadi Simba na Yanga ikiwa imekaribia huku wale wa Yanga wakihisi kufanyiwa hujuma ili mchezaji huyo aikose mechi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka