Connect with us

Soka

Morrison Apaa Kuivaa Kagera sc

Winga wa Yanga Bernard Morrison ‘amepaa’ kuelekea Bukoba tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Alhamisi, Julai 09 kwenye uwanja wa Kaitaba.

Morrison ataungana na wachezaji wengine ambao jana walicheza na Biashara United kule Mara ambapo Hata hivyo Eymael aliahidi kuwa Morrison ataungana nao Bukoba.

Kocha Luc Eymael hakumjumuisha Morrison kwenye safari ya Musoma kwa kile alichokieleza kumpa nafasi mchezaji huyo kuweka sawa mambo yake na uongozi wa Yanga.

Mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakuwa maandalizi ya mwisho ya kikosi cha Yanga kabla ya mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili ijayo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka