Connect with us

Soka

Mo Atuliza Hali ya Hewa

Muwekezaji wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji ni kama ametuliza hali ya hewa baada ya kuthibitisha kuwa Staa Cletous Chama ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia katika klabu hiyo mpaka mwaka 2022.

Mo dewji alisema hayo baada ya kuwa na kelele za muda kutoka kwa watani wa jadi ambao walijinasibu kumsainisha kiungo huyo mwenyeji wa ndola nchini Zambia.

Pia tajiri huyo namba moja nchini kwa mujibu wa jarida la Forbes amethibitisha kuhusu timu hiyo kutomhitaji kiungo Mukoko Tonombe wa Yanga sc huku kwa maana bado suala la mchezaji huyo halijafika katika kamati ya usajili ya timu hiyo hivyo ni propaganda tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka