Nyota wa Yanga kijana Mapinduzi balama sasa wanamuita “kipenseli” ni kijana mzaliwa wa mkoa wa Iringa. ni moja kati ya wachezaji wenye viwango bora kabisa nchini.
Mchezaji huyu ni moja ya usajili bora ndani ya Yanga kwa msimu huu kwani anajituma na kupaambana uwanjani mwanzo mwisho.
Mapinduzi alisajiliwa na Yanga akitokea Alliance fc ya Mwanza.
ALLIANCE WALIMTOA WAPI???
Klabu ya Alliance ilikuwa na mchezo wa kirafiki mkoani Iringa na timu inayoitwa Mtwivila fc,ndipo Balama akaonekana .
Kwenye mchezo huo Balama alikuwa haeleweki anacheza namba ngapi ndani ya uwanja kwani alikuwa anaonekana wakati wa kuzuia,kuanzisha mashambulizi na hata kushambulia kabisa.
Wachezaji wa Alliance walisumbuliwa sana na kijana huyu kwani alicheza kwa kiwango bora kabisa kwenye mechi hiyo.
Matokeo ya mechi hiyo ya kirafiki Alliance waliibuka na ushindi wa mabao 8~1 na hilo bao moja la Mtwivila fc lilifungwa na Mapinduzi Balama.
Baada ya mechi hiyo Alliance walirejea mkoani Mwanza ndipo wakaanza mchakato wa kumleta Balama ndani ya kikosi chao.
Hata baadhi ya wachezaji ndani ya Alliance waliushauri uongozi ili wamsajili haraka Balama kwani ni mchezaji ambaye alifanya vizuri kwenye mchezo ule wa kirafiki.
BALAMA AANZA MAISHA NDANI YA ALLIANCE.
Hatimaye Alliance walimchukua Balama na akiwa ndani ya Alliance aliwasha moto kuzidi ata kiwango alichokionyesha kwenye mechi ya kirafiki nadhani waliokuwa wakifatilia michezo ya ligi kuu ambayo Alliance ilicheza baasi waliona kiwango chake.
YANGA YAMSAJILI.
Klabu Ya Yanga ilimsajili kwa mkataba wa miaka mitatu
Namba halisi ya Balama ni namba nane au kumi lakini ndani ya Yanga mara kadhaa alichezeshwa kama winga wa kulia na hata beki wa kulia na bado alionyesha kiwango bora.
Klabu ya Alliance baada ya kuona Yanga haimtumii ipasavyo nyota huyo uongozi uliwahi kutamka kuwa wanatamani warudishiwe nyota
huyo na Yanga wapewe pesa zao kwani hawautumii vyema uwezo wa Balama japo mashabiki wa Yanga wanaona alikuwa bora tangu asajiliwe.
Baada ya kuja Mkwasa ameanza kumchezesha kwenye nafasi sahihi tutarajie kuona mengi kutoka kwake.
Credit:Daud Lwena(Daud Yanga)