Connect with us

Soka

Misumari Yamchosha Bigirimana

Kiungo mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga sc Issa Bigirimana amedai halioni lango anapokua anaichezea klabu hiyo kutokana na kupigwa misumari (Kurogwa) na mchezaji mwenzake wa timu hiyo.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Apr ya nchini Rwanda amefunguka hayo baada ya kushindwa kuonyesha kiwango mazoezini na kutopata nafasi katika michezo mbalimbali ya klabu hiyo huku akiandamwa na majeraha ya nyama za paja.

Bigirimana raia wa Burundi amedai kuna mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji amekua akimfanyia vitendo hivyo ili asipate nafasi ya kucheza klabuni hapo.

Kocha Mwiny Zahera hakupatikana alipotafutwa na Sportsleo ili kujibu tuhumu hizo za mambo ya ushirikina kikosini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka