Connect with us

Soka

Miraji Akwaa Tuzo Vpl

Mshambuliaji wa timu ya Simba sc Miraji Athuman ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania bara kwa mwezi Septemba  akiwashinda Meddie Kagere na Ismail Kada wa Prisons ya Mbeya.

Kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini (Tff) Miraji ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisadia timu ya Simba kushinda michezo minne ya ligi iliyocheza mpaka sasa huku akifunga mabao mawili na kusaidia upatikanaji wa mabao mengine mawili kwa mwezi  septemba pekee.

Miraji aliisaidia Simba kupata alama tatu mbeli ya Mtibwa Sugar baada ya kushinda 2-1 huku wakishinda 3-0 dhidi ya Kagera sugar na 2-0 dhidi ya Biashara United.

Miraji alikulia akademi ya Simba sc kasha baadae alicheza timu kadhaa ikiwemo Toto Afrika na baadae akaenda Lipuli Fc kisha akasajiliwa Simba ambapo hakutegemewa kufanya vizuri mbele ya mastaa kama Ibrahim Ajib,Deo Kanda na wengine.

Kutokana na tuzo hiyo mchezaji huyo atajipatia fedha Taslimu za kitanzania shilingi milioni moja na kisimbuzi cha Azam Tv.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka