Connect with us

Soka

Mexime Akubali Mziki wa Simba sc

Kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime ameukubali uwezo wa kikosi cha Simba baada ya kufungwa mabao 3-0 katika uwanja wa nyumbani wa Kaitaba uliopo mjini Bukoba mkoani Kagera mchezo uliofanyika jana.

Awali kocha  huyo alijitapa atawafunga Simba sc akiringia rekodi yake ya msimu uliopita alopowafunga wanamsimbazi hao mechi zote za nyumbani na ugenini.

Tambo hizo zilikoma baada ya dakika 90 za mchezo huo kufuatia mabao ya Meddie Kagere aliyefunga mawili na Mohamed Hussein yaliyoipa pointi tatu simba ugenini.

“Simba ni timu bora sio tu ndani ya nchi bali hata Afrika ukitaja timu bora nne simba itakuwemo,lSisi tulifanya makosa kadhaa na wenzetu wameyatumia”.Alisema Mexime

Kagera ilikua imeshinda mechi zote za awali na kuwafanya kuongoza ligi kwa kuwa na pointi tisa kabla ya jana kukubali kipigo hicho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka