Connect with us

Soka

Mendy aandamwa na kesi za ubakaji

Beki wa kushoto wa Manchester City Benjamin Mendy amekutwa na kosa lingine la ubakaji katika mfululizo wa mashtaka hayo na kufanya kufikia saba hadi sasa huku linguine moja likiwa ni la unyanyasaji wa kingono.

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa anayeishi mtaa wa Prestbury katika kitongoji cha Chesire Jijini Manchester alikutwa na kosa hilo wiki iliyopita lakini hakusomewa kutokana na vikwazo vya kusafiri kutokana na ugonjwa wa Uviko-19,baada ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo mchezaji huyo alionekana katika mahakama Chester Crown kusikiliza mashtaka hayo.

Tukio hili la sasa la ubakaji linatajwa kutokea mwezi Julai mwaka huu huku mengine ya awali yakitokea kati ya Oktoba 2020 na Agosti 2021.

Beki huyo maarufu kwa matumizi ya mitandao ya kijamii anashikiliwa mahabusu na jeshi la polisi la Manchester tangu mwezi Agosti mwaka huu na atasalia huko hadi kesi yake itakaposomwa tena Januari mwakani.

Mendy alijiunga na Manchester City mwaka 2017 akitokea Monaco ya Ufaransakwa dau la paundi milioni 40 na tangu kujiunga kwake amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya ligi kuu licha ya kutokuwa sehemu ya kikosi mara kwa mara kutokana na kutumia muda mrefu kwenye meza ya matibabu akiuguza majeraha.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka