Connect with us

Soka

Mbeya City Yamfungua Mdomo Nahodha Yanga

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbea City hawakuyatarajia, lakini ndivyo mpira ulivyo.

Katika mchezo huo ambao Yanga ilitawala kila idara, ilitengeneza nafasi nyingi lakini waliweza kutumia nafasi moja tu.

“Dah! sijui hata niseme nini ila acha tumuachie yeye mwenyewe muumba sababu alishapanga iwe vile”

“Hapo ndipo utakapojua mchezo wa mpira una matokeo ya kikatili.. lakini tunakushukuru mungu wetu hata kwa hiki kidogo ulichotupatia inshaallah,” ameandika Abdul kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Kwenye mchezo huo bao la Yanga lilifungwa na Bernard Morrison lakini likipita mguuni kwa Abdul ambaye msimu huu amerejea kwenye makali yake

Abdul amehusika kwenye mabao matano ya Yanga mpaka sasa msimu huu katika michezo ya ligi kuu

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka