Connect with us

Soka

Matola Huyoo Simba

Kocha wa timu ya Polisi Tanzania Selemani Matola anaelekea kujiunga na timu ya Simba sc baada ya kuomba kuvunja mkataba na timu hiyo ambayo makao makuu yake yako mkoani Kilimanjaro nchini.

Matola anatajwa kwenda Simba kuchukua nafasi ya kocha Dennis Kitambi ambaye anaondolewa baada ya klabu hiyo kuamua kuvunja benchi lote la ufundi huku ikiwa tayari imempa mkono wa kwaheri kocha mkuu Patrick Aussems.

“Kwa sasa tunashughulikia ombi lake la kuvunja mkataba maana lina hatua kadhaa za kuzifuata na tukimaliza ndio tutajadili majina yaliyopendekezwa mezani juu ya nani awe kocha msaidizi”.Alisema Frank Godfrey kaimu katibu mkuu wa timu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka