Connect with us

Soka

Mastaa 8 Kuwakosa Ndanda

Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara , Yanga SC kesho wanashuka kwenye dimba la Nangwanda Sijaona Mtwara kuvaana na Ndanda SC huku wakikosa huduma za wachezaji wao wanane kutokana na sababu tofauti.

Wachezaji hao ni Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Lamine Moro, Juma Balinya, Ali Ali, Maybin Kalengo, Paul Godfrey na Cleofas Sospeter.

Kwa mujibu wa meneja ambaye pia ni mratibu wa timu hiyo Dismas Ten, Feisal Salum amepewa ruhusa maalum ya kwenda kumuuguza mzazi wake, na wengine saba wanakosekana kutokana na kuwa majeruhi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka