Connect with us

Soka

Mashabiki Ruksa Viwanjani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Tamaduni na Michezo Dk.Hassan Abassi ameruhusu mashabiki kuingia uwanjani katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13.

Licha ya kutoa agizo hilo pia amebadili uamuzi wa awali ambao ulielekeza ligi hiyo kuchezwa kituo kimoja lakini sasa itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini kama ilivykua awali kabla ya janga la Corona.

Awali Serikali kupitia kwa Wizara ya Michezo ilizuia mechi zote za ligi kuu Tanzania pamoja na michezo mingine ili kudhibiti kusambaa kwa Virusi vya Corona lakini kutokana na kupungua kwa maambukizi Serikali imeamua kurudisha michezo lakini kwa kufuatia muongozo wa wizara ya afya kuhusu jinsi ya kudhibiti Corona.

KUHUSU MASHABIKI

Pia katibu mkuu huyo ameruhusu mashabiki kuingia uuwanjani hasa katika mechi zenye idadi ndogo ya watazamaji ambao watakaa katika mtindo wa mita moja huku zile ambazo zina mashabiki wengi watatakiwa kuingia nusu ili kuzingatia taratibu za Wizara ya Afya jinsi ya Kujikinga na Corona.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka