Connect with us

Soka

Manyika Amfungukia Kindoki

Kocha mpya wa makipa wa klabu ya Yanga sc Peter Manyika amemzungumzia uwezo wa kipa mkongomani wa klabu hiyo Klaus Kindoki baada ya kumfundisha mazoezini kwa siku kadhaa.

Manyika kipa wa zamani wa Yanga na timu ya taifa amesema kiwango cha kipa huyo kinaridhisha japo amemueleza makosa yake ambayo inabidi ayafanyie kazi kama kocha ili kuhakikisha kiwango cha kipa huyo kinaboreka zaidi na kurudisha upendo kwa mashabiki.

“Nimeongea nae na amenieleza changamoto zake ambazo nimeanza kuzifanyia kazi na zinafundishika na nampongeza kwa kukubali makosa yake anaonekana anapenda mafanikio kwani ni muwazi kwa kila kitu”.

Manyika amepewa kazi ya kuwanoa makipa wa Yanga baada ya kuwa na malalamiko kutoka kwa magolikipa wa timu hiyo kuhusu ufundishaji wa kocha Juma Pondamali ambaye amefungiwa virago.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka