Connect with us

Soka

Manula,Kakolanya Watemwa Stars

Makipa wa klabu ya Simba sc Aishu Manula na Beno Kakolanya wameachwa katika kikosi cha timu ya taifa (Taifa stars) kilichochaguliwa kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya Sudan.

Kikosi hicho kitachoongozwa na kaimu kocha mkuu Ettiene Ndayiragije na wasaidizi Juma Mgunda na Seleman Matola kimetangazwa huku nafasi za makipa hao zikichukuliwa na Juma Kaseja na Metacha Mnata ambao wamekua na viwango vizuri siku za karibuni.

Pia katika kikosi hicho wachezaji Mzamiru Yassini na Miraji Athuman kutoka Simba sc wameitwa kufuatia kufanya vizuri katika michezo ya klabu yao huku Miraji akiwa amecheza michezo miwili na kufunga mabao mawili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka