Connect with us

Soka

Manara Ahimiza Ushirikiano

Mkuu wa idara ya habari ya Simba sc Haji Manara amehimiza ushirikiano wa mashabiki wa soka nchini kuelekea katika michezo ya marudiano ya klabu bingwa Afrika na ile ya kombe la shirikisho.

Manara amesisitiza hayo kuelekea katika mechi hizo ambapo Azam itavaana na Fasil Kanema ya Ethiopia huku Kmc itawakaribisha As Kigali katika mechi za marudiano zitakazo fanyika nchini huku Simba ikiwakaribisha Ud Songo katika ligi ya mabingwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari pia manara amesisitiza umuhimu wa mashabiki kusapoti timu za nyumbani bila kujali ni timu gani inacheza bali kuweka mbele utaifa.

Simba inajiandaa na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam fc mchezo utakaopigwa siku ya jumamosi saa moja usiku.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka