Connect with us

Soka

Man city Kifungoni

Klabu ya soka ya Manchester City ya nchini England, imefungiwa kwa miaka miwili kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Adhabu hiyo imetolewa na Shirikisho la soka barani Ulaya “UEFA”, baada ya timu hiyo kukutwa na hatia ya ukiukwaji wa Sheria ya matumizi mabaya ya fedha ya “Uefa Financial Fair Play.”

Baada ya uchunguzi uliofanywa na bodi ya Financial Fair Play ya Uefa (CFCB) City walikutwa na hatia, huku matukio hayo yakiripotiwa kufanywa kati ya mwaka 2012 na 2016.

Pia mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini England, wamepigwa faini ya Euro milioni 30 huku Adhabu hiyo itaanzia kuanzia msimu wa 2020/21 na 2021/22.

Hata hivyo City wamepanga kukata rufaa katika mahamaka ya usuluhishi wa michezo “CAS”.

Cc:Morosports

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka