Connect with us

Soka

Makambo Anukia YANGA

Habari ya mjini ni kwamba yule straika anayefunga kwa kichwa na miguu yote Heritier Ebenezer Makambo anarudi Jangwani baada ya kuuzwa msimu uliopita katika klabu ya Horoya Fc ya nchini Guinnea.

Makambo aliyekuwa mfungaji bora katika kikosi cha Yanga msimu uliopita huku kwenye ligi akizidiwa na Meddie Kagere  wa Simba na Salim Aiyee aliyekua anaichezea Mwadui Fc.

Taarifa za ndani zinadai klabu hiyo kupitia kwa wadhamini wake kampuni ya Gsm tayari wameshakubaliana maslahi binafsi na mshambuliaji huyo na kilichobaki ni mazungumzo na klabu yake kuhusu kununua mkataba wake au kumchukua kwa mkopo.

Kwa  mujibu wa ripoti ya kocha wa klabu hiyo Luc Eymael anahitaji mshambuliaji wa maana baada ya waliokuwepo wakiongozwa na David Molinga na Yikpe Gnamien kuchemka na wanatarajiwa kupewa mkono wa kwaheri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka