Connect with us

Soka

Majanga Yamuandama Guardiola

Ni kama mkosi umemuandama Pep Guardiola na timu yake ya Manchester city baada ya kuandamwa na majeruhi katika wachezaji wanaocheza nafasi muhimu katika kikosi hicho.

Baada ya wiki iliyopita kumkosa beki wake Aymetic Laporte kwa majeraha yatakayomfanya akae nje kwa muda miezi minne sasa imeripotiwa beki muingereza John Stones nae amepata majeraha na atakaa nje kwa muda wa  wiki 4 mpaka 4.

Majeraha hayo yanamfanya kocha huyo kubakiwa na beki asili wa kati mmoja ambaye ni Nicolaus Otamendii huku akilazimika kumchezesha mbrazil Fernandinho katika nafasi hiyo huku pia akiwa hana budi kuwapandisha makinda Javi Garcia na  Taylor Harwood-Bellis katika kikosi cha kwanza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka