Connect with us

Soka

Madrid Achezea Kichapo kwa Atletico

Timu ya Atletico Madrid imeibuka na ushindi mnono wa magoli 7-3 dhidi ya mahasimu Real Madrid katika michuano ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi mbalimbali ulaya (Icc championship) katika mechi iliyochezwa New Jersey nchini Marekani.

Diego Costa alifunga magoli manne dakika ya 1,28,45 na 51 huku mabao mengine ya vijana wa Diego Simeone yakifungwa na Joao Felix 8′,Correa dk 19′ na Vitolo dk 70′ na kuwafanya Atletico kuibuka na ushindi huo mnono huku mabao ya Real Madrid yakifungwa na Nacho 59′,Benzema 85′ na J.Hernandez dk ya 89.

Licha kufunga mabao manne Diego Costa alitolewa mchezoni dakika ya 65 baada ya refa kumuonyesha kadi nyekundu baada ya kupigana na Dani Calvajal na refa kuwatoa mchezoni wote wawili.

“Tulianza mchezo vibaya,ni mechi ya levo za juu na tulianza vibaya” alisema kocha Zinedine Zidane baada ya mechi wakati akifanya mahojiano na vyombo vya habari.

“Tulijiandaa kwa mechi na tulifahamu tutapeleka maafa kwa wapinzani wetu,Tulikua na mchezo mzuri”.alimalizia kocha huyo mwenye mbwembwe raia wa Ajentina.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka