Connect with us

Soka

Mabadiliko Yanga Kukamilika Mei

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo utakamilishwa mwezi Mei mwaka huu.

Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku kubwa kuona jambo hilo likitokea ambapo Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka Wanachama wa klabu hiyo wakae tayari kupokea mabadiliko hayo.

“Tumeunda Kamati ambayo inasimamia mchakato huo, tunashukuru kila kitu kinaenda sawa, ” amesena

“Tumekuwa tukipokea maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali. Muhimu zaidi tumepata nafasi ya kwenda kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa”

“Lengo letu ni kuwa na mfumo ambayo utaifanya Yanga isimame na kuweka historia ya Mafanikio”

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo mwaka uliopita, Dk Mshindo Msolla alitangaza suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kuwa kipaumbele chake cha kwanza

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kujaribu kubadili mfumo wake wa uendeshaji kuwa kampuni Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 Yanga imejaribu mara kadhaa bila ya mafanikio, mivutano baina ya wanachama ikikwamisha zoezi hilo

Lakini hitaji la mabadiliko wakati huu limekuwa kubwa miongoni mwa Wanachama wa klabu hiyo

Kama mpango huo utafanikiwa, Dk Msolla ataingia kwenye historia ya klabu hiyo kwa kufanikiwa kumaliza mchakato huo ambao watangulizi wake hawakufanikiwa kuukamilisha

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka