Connect with us

Soka

Lusajo Aiweka Njia Panda Namungo

Nahodha  wa Namungo Reliant Lusajo ameiweka njia panda klabu yake ya Namungo Fc baada ya kugoma kusaini mkataba mpya huku akitoa masharti ya kutimizwa.

Klabu hiyo ilifanya mazungumzo na meneja wa mchezaji huyo lakini walishindwa kufikia muafaka hivyo kuleta sintofahamu ukizingatia timu kama Yanga sc na Simba sc zinamnyemelea staa huyo mwenye mabao 11 ya ligi kuu.

Hata hivyo taarifa za ndani ya Namungo zinasema tayari kocha Hitimana Thierry ameshapata mbadala wa mshambuliaji huyo pamoja na Bigirimana Blaise kama wakiamua kuondoka mwishoni mwa msimu ambapo mikataba yao itakua inafikia mwishoni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka