Connect with us

Soka

Lukaku Amtuliza Ibrahimovich

Kikosi cha Inter Milan kimeibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya mahasimu wao, AC Milan katika mchezo wa ligi kuu nchini Italia(Serie A)

Zlatan Ibrahimovic, ambaye amerejea katika ligi kuu ya Italia hivi karibuni, aliifunga timu yake zamani ya Inter (45′) na kutengeneza goli lingine lililofungwa na Ante Rebic (40′), na kufanya hadi halftime, AC Milan, kuongoza kwa magoli 0-2.

Kipindi cha pili Inter waliamka na Marcelo Brozovic na Matias Vecino, waliifungia Milan magoli ya haraka katika dakika ya 51′ na 53′, na kufanya ubao usome 2-2.

Vijana hao wa Antonio Conte walichukua uongozi dakika 20 baadae, baada ya beki, Stefan De Vrij kufunga goli kwa kichwa, kabla ya nyota wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, kupigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 90.

Inter wamefikisha alama 54 katika msimamo wa ligi ya Serie A, wakiwa alama sawa na vinara wa ligi hiyo kibibi kizee cha Turin,Juventus

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka