Connect with us

Soka

Luc Awatema Manyika,Mkwasa

Kocha mkuu wa Yanga SC, Luc Aymael amekataa kusafiri na makocha wa Yanga Boniface Mkwasa ambaye ni kocha msaidizi na Peter Manyika ambaye ni kocha wa magolikipa kwenda Morogoro na Iringa kwa ajili ya mechi mbili za mwisho wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na Lipuli FC.

Hivi karibuni kocha huyo alikataa kufanya kazi na makocha hao na Sasa amesafiri na kocha wa viungo Rido Birdien  na Said Maulid kocha wa kikosi cha cha vijana(U20).

Taarifa zinadai kocha huyo amegoma kufanya kazi na wasaidizi hao akishinikiza kuruhusiwa kutafuta wasaidizi wake mwenyewe huku pia tayari ikidaiwa amemchangua kocha wa klabu ya Namungo Fc Hitimana Thiery kuja kumsaidia msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka