Connect with us

Soka

Lindeloff Ajifunga Minne United

Beki mswedeni wa Manchester united Victor Lindeloff amesaini mkataba mpya wa miaka minne wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi kuendelea kusalia Old Trafford mpaka msimu wa 2024.

Beki huyo aliyesajiliwa kutokea Benfica msimu wa 2017 mpaka sasa ameichezea united michezo 74 huku kwa upande wa timu ya taifa ya Sweden akicheza mechi 31.

“Nina furaha toka nijiunge na timu hii nimejisikia nipo nyumbani na nimekua kama mchezaji na kinafsi kwa kipindi cha miak miwili hapa na ninamshukuru kila mtu kwa sapoti anayonipa”Alisema beki huyo.

United chini ya kocha Olle Gunnar Solskjaer imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji kama David De Gea na sasa imemuongezea beki huyo huku juhudi zikiendelea kumshawishi kiungo Paulo Pogba kuongeza mkataba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka