Connect with us

Soka

Lampard Hali Tete

Licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu ugenini dhidi ya Wolves kocha wa Chelsea Frank Lampard ana wakati mgumu kutokana na mastaa takribani nane wa kikosi cha kwanza kuwa majeruhi.

Mastaa hao wakiongozwa na Ngolo Kante na Antonia Rudger ambao wamepata majeraha hivi karibuni huku beki wa kushoto Emerson naye ameongezeka baada ya kupata tatizo la misuli katika mchezo wa Italia dhidi ya Finland.

Wengine ni Callum Hudson-Odoi,Ruben Roftus Cheek,Mateo Kovacic,Pedro Rodriguez,Reece James ambao wanamatatizo mbalimbali yanayowafanya wasiwe fiti kuwavaa Wolves huku ikitarajiwa baadhi yao wanaweza kuwahi mechi hiyo japo hawawezi kupambana kwa dakika zote tisini.

Chelsea imekua na mwendo wa kusuasua kutokana na kutofanya usajili wa kutosha baada ya kupewa adhabu na shirikisho la soka duniani(Fifa) ya kutosajili huku ikiwa imecheza jumla ya mechi 4 wakiwa wamecheza kwenye ligi kuu ya uingereza wakishinda moja na kufungwa moja huku mechi mbili wakitoa sare.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka