Connect with us

Soka

Kocha Yanga Afunga Ndoa

Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Luc Eymael leo amefunga ndoa ya kimya kimya na mpenzi wake Patricia Abbruzzese nchini Afrika Kusini kutokana na mlipuko wa homa ya virusi vya Corona.

Eymael amesema ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Harre nchini humo lakini ilikuwa binafsi kwakua hakuruhusiwi mikusanyiko yoyote.

Kocha huyo ameiambia Wapendasoka kuwa baada ya kupata nafasi katika kipindi ligi imesimama akaona amalize kabisa suala la ndoa.

“Ni kweli nimefunga ndoa lakini ilikuwa ni binafsi kwakua kuna mlipuko wa virusi vya Corona, tulienda kanisani tu tumemaliza tunashuru,” alisema Eymael.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka